Guaido aitisha maandamano zaidi Venezuela

Juan Guaido, aliyejitangaza rais wa mpito nchini Venezuela, amewatolea wito wafuasi wake kuendelea kuandamana dhidi ya Rais Nicolas Maduro, baada ya maandamano ya jana yaliyokumbwa na ghasia.

Akizungumza kupitia mkanda wa video uliowekwa mtandaoni, Guaido amesema kile anachokiita ”Operesheni Uhuru” kitaendelea, na kulitaka jeshi kupiga hatua mbele katika juhudi za kumpindua Maduro.

Mpango wa Guaido wa kuonyesha kuwa amejishindia uungwaji mkono wa jeshi uliishia katika vurugu katika mitaa ya mashariki mwa mji mkuu, Caracas. Baadaye Rais Maduro alizungumza kwa njia ya televisheni, akivipongeza vikosi kwa kuzima alichokiita ‘jaribio la mapinduzi’.

Maduro amesema matukio hayo hayatakwepa mkono wa sheria, akiapa kuwa waliotenda uhalifu dhidi ya katiba watafunguliwa mashtaka.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kupitia ujumbe wa mtandao wa Twitter, kwamba Marekani inasimama pamoja na watu wa Venezuela wanaotaka uhuru.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.