Naruhito atawazwa mfalme mpya Japan

Mfalme mpya wa Japan, Naruhito, amechukua nembo za ufalme kama alama rasmi ya kurithi uongozi kutoka kwa baba yake Akihito aliyeng’atuka jana. Nembo hizo ni pamoja na upanga, vito na muhuri wa ufalme.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa, Naruhito ameahidi kutekeleza majukumu yake kama alama ya taifa la Japan na watu wake, kama inavyoelezwa katika katiba ya taifa hilo. Alisema atazingatia urithi wa baba yake wa kujitolea kwa ajili ya amani na kuwa karibu na watu, na kuongeza kuwa anaelewa vyema uzito wa majukumu aliyokabidhiwa.

Mfalme Naruhito mwenye umri wa miaka 59 ni msomi aliyepata elimu yake ya juu katika chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza.

Mke wake, Masako na binti yao, Binti Mfalme Aiko hawakushiriki katika sherehe ya kutawazwa kwake, kwa sababu katika mila za Kijapani sherehe hizo huhudhuriwa tu na wanaume wa makamo.

Chanzo: Mtandao wa Idhaa ya Kiswahili ya DW

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.