Semenya ashindwa rufaa dhidi ya IAAF kuhusu homoni

Caster Semenya ameshindwa katika kesi muhimu dhidi ya Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF), hii ikimaanisha kuwa shirika hilo litaruhusiwa kudhibiti viwango vya homoni za wanariadha wa kike.

Mahakama ya Utatuzi wa Migogoro Michezoni (CAS) imekataa kesi ya Afrika Kusini ya kupinga sheria mpya za IAAF.

Lakini CAS ilisema kuwa ilikuwa na “hofu kubwa juu ya utekelezwaji wa baadaye” wa sheria hizo mpya.

Semenya, mwenye umri wa miaka 28, alisema sheria hizo” si za haki ” na kwamba alitaka “kukimbia kama nilivyo, jinsi nilivyozaliwa”.

Sasa mshindi huyo wa Olimpiki, dunia na mashindano ya Jumuiya ya Madola kwa mita 800 pamoja na wanariadha wengine wenye jinsia zaidi ya moja (DSD) watalazimika kupata matibabu ili kushiriki mashindano ya kuanzia mbio za mita 400 hadi maili au wabadili mbio.

CAS ilibaini kuwa sheria zilizokuwepo za wanariadha wenye DSD zilikuwa ni za kibaguzi, lakini kwamba ubaguzi huo ulikuwa “muhimu, wa kueleweka na wa uwiano kwa ajili ya kulinda maadili ya wanariadha wanawake”.

Hata hivyo, CAS ilielezea hofu kubwa juu ya ya utekelezwaji wa sheria ikiwemo:

  • Hofu kwamba wanariadha wanaweza kukiuka masharti ya viwango vya homoni za kike vilivyowekwa na IAAF;
  • Maswali kuhusu faida za viwango vya juu homoni za jinsia tofauti wanazozipata wakimbiaji wa mita 1500 na maili.
  • Utekelezaji wa wanariadha wa sheria hizo mpya

CAS imeitaka IAAF kuangalia uwezekano wa kuchelewesha utekelezwaji wa sheria hizo kwa wanariadha wanaokimbia katika matukio ya mita 1500 na maili moja hadi pale ushahidi utakapopatikana.

Semenya hatatakiwa kupunguza viwango vyake vya homoni za (testosterone) kama alikamilisha hilo katika mbio za Diamond Ligi mjini Doha, Ijumaa.

Katika ujumbe wake wa Twitter kufuatia uamuzi wa CAS, Semenya amesema kuwa ”Wakati mwingine ni bora kujibu kwa kutojibu lolote.”

Chanzo: Mtandao wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.