Waandamanaji Sudan wasema jeshi halina nia ya kukabidhi madaraka kwa raia

Waandamanaji nchini Sudan wamelishutumu jeshi la nchi hiyo kutokuwa na nia ya dhati ya kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia, baada ya kuangushwa kwa utawala wa Rais Omar al-Bashir.

Waandamanaji na wanaharakati wamekuwa wakifanya mazungumzo na Baraza la Mpito la Kijeshi, kwa lengo la kuunda baraza la pamoja litakaloongozwa na raia, ambalo litasimamia kipindi cha mpito.

Hata hivyo, mazungumzo hayo yamekwama, kutokana na tofauti kuhusu upande unaopaswa kuwa na wajumbe wengi zaidi katika baraza hilo.

Katika ishara ya kushamiri kwa mzozo huo, hapo jana waandamanaji walizifunga barabara kaskazini mwa mji mkuu, Khartoum, kwa kutumia miamba na kuchoma moto matairi, hivyo vikiwa vitendo vya kwanza vya namna hiyo tangu kupinduliwa kwa al-Bashir.

Wakati huo huo, Umoja wa Falme za Kiarabu umesema nchi za Kiarabu zinaunga mkono kipindi cha mpito kinachoweka uzani baina ya matakwa ya umma wa Sudan na uthabiti wa kitaasisi.

Chanzo: Mtandao wa Idhaa ya Kiswahili ya DW

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.