Amref Health Africa yazinduwa mradi wa Afya Kamilifu Zanzibar

Shirika la Amref Health Africa limezinduwa mradi wake mpya unaolenga  kupanuwa  juhudi za kutowa huduma za matunzo na matibabu ya kufubaza Virusi vya Ukimwi (VVU) visiwani Zanzibar na katika mkoa wa Tanga, likiungana na juhudi zinazoendelea duniani kote zikiwa na lengo la kumaliza  janga la Ukimwi ifikapo 2030.

Mradi huo uliopewa jina la ‘Afya Kamilifu’ ni wa miaka mitano, ukifadhiliwa na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani Kupambana na Ukimwi (PEPFAR) kupitia  Kituo cha Kudhibiti  Magonjwa (CDC) nchini Tanzania.

Mradi wa Afya Kamilifu utatekelezwa kwa ushirikiano na kupata miongozo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto upande wa Tanzania Bara na wizara za Afya na na Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) kwa upande wa Zanzibar.

Mradi huu unaotekelezwa Tanzania Bara na Zanzibar unaunga mkono malengo mapya ya programu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa kuhusu VVU/Ukimwi ya 95-95-95 inayomaanisha kwamba ifikapo mwaka 2030, asilimia 95 ya watu wenye VVU wajue hali zao za VVU, wakati ambaoo asilimia 95 ya wanaojua hali zao ya VVU wawe wakipata matibabu na kwamba asilimia 95 ya hao wanaopata matibabu wawe wameupunguza kasi mzigo wao wa virusi mwilini.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.