Bashir sasa kuhojiwa kwa utakishaji fedha na kufadhili ugaidi

Mwendesha mashitaka mkuu nchini Sudan ameamuru kuhojiwa kwa Rais aliyeondolewa madarakani, Omar al Bashir, kuhusu madai ya “utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi”.

Chini ya utawala wa Bashir, Sudan iliwekwa kwenye orodha ya Marekani ya mataifa yanayofadhili ugaidi kutokana na mahusiano yake na kundi la itikadi kali.

Muasisi wa al-Qaeda Osama bin Laden, aliyehusika na mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 mijini New York na Washington mwaka wa 2001, aliishi Sudan kati ya mwaka wa 1992 na 1996.

Jenerali Abdel-Fattah Burhan, mkuu wa baraza la kijeshi, alisema mwezi uliopita kuwa zaidi ya dola milioni 113 pesa taslimu zilipatikana katika makazi ya al-Bashir.

Amri hiyo ya kaimu mwendesha mashitaka mkuu Al Waleed Sayyed Ahmed imetolewa wakati mamia kwa maelfu ya waandamanaji wakiendelea kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi kulitiaka likabidhi madaraka kwa raia.

Al Bashir aliondolewa madarakani na kukamatwa na jeshi la Sudan mnamo Aprili 11 baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya kupunga utawala wake wa miaka 30.

Jeshi na viongozi wa upinzani sasa wanafanya mchakato wa kuunda serikali ya mpito.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.