Rais amfuta kazi mkuu wa polisi

Rais Nicos Anastasiades wa Cyprus amemfuta kazi mkuu wa polisi wa nchi huyo, wakati shinikizo likizidi juu ya namna serikali ilivyochelewa kushughulikia mauaji ya wanawake na wasichana saba wa kigeni.

Barua ya rais huyo kwa Mkuu wa Polisi Zacharias Chrysostomou imemueleza kuwa ajira yake itazingatiwa imefutwa kufikia tarehe 7 Mei.

Anastasiades amesema uamuzi wake unatokana na kile kinachoonekana kuwa ni dharau na uzembe wa polisi kwenye uchunguzi wa watu waliopotea.

Tangazo hili la rais linakuja siku moja tu baada ya waziri wa sheria, Ionas Nicolau, naye kuamua kujiuzulu kutokana na kadhia hiyo, ambayo ilifichwa kwa takribani miaka mitatu.

Mtuhumiwa aliyetambuliwa kama afisa wa kijeshi mwenye umri wa miaka 35, Nicos Metaxas, amekiri kuhusika na vifo vyote saba, vilivyopewa jina la mauaji ya kwanza ya mfululizo kwenye kisiwa hicho cha Bahari ya Mediterenia, mashuhuri kwa utalii.

Waliouawa walikuwa raia wa Ufilipino na Nepal.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.