Mwanamuziki Mose Fan Fan afariki dunia

Mwanamuziki maarufu nchini DR Congo, Mose Fan Fan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75. Mwanamuziki huyo alikufa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa huenda ni mshtuko wa moyo nyumbani kwake karibu na barabara kuu ya Thika jijini Nairobi, Kenya.

Mtunzi huyo wa wimbo ‘Papa Lolo’ uliotia fora alikuwa mjini Nairobi katika mradi wa kurekodi nyimbo mpya na wanamuziki wa Nairobi akiwemo Paddy Makani na Disco Longwa.

”Mose alikuwa akicheza Gita na bendi ya Franco Ok Jazz mwaka 1972. Ninamtambua kuwa mchezaji Gita na mwandishi mzuri wa nyimbo barani Afrika . Amekuwa akizuru Nairobi mara kwa mara tangu 2015 akishirikiana na bendi ya Ketebul Music na Tabu Osusa,” alisema mshindi wa tuzo ya kuchora wanasesere, Paul Kelemba (Mado) kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya.

Na mashabiki wa mwanamuziki huyo waliomboleza kifo chake muda tu habari zake zilipoanza kusambaa katika vyombo vya habari.

Chanzo: Idhaa ya Kiswahili ya BBC

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.