ACT yaadhimisha miaka 5 kwa wito wa umoja wa wapinzani

Chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania kimeadhimisha hivi leo miaka mitano tangu kupata usajili wa kudumu kwa kutoa wito wa kuundwa kwa umoja mkubwa kabisa wa upinzani ili kukiondowa chama tawala, CCM, madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi Kuu za chama hicho Mjini Zanzibar, Naibu Kiongozi Juma Duni Haji alisema kuwa baada ya miaka takribani minne ya utawala wa Rais John Magufuli, Watanzania wametambuwa kuwa CCM haina nia wala uwezo wa kuwaletea maendeleo yoyote, isipokuwa tu kuwakandamiza na kuuwa uchumi.

“Chama cha ACT Wazalendo kinafahamu kuwa kinao wajibu mkubwa wa kihistoria wa kuitoa CCM madarakani 2020 kwa upande wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wajibu huu utawezekana, kwa sababu CCM imeshindwa kuendesha nchi na hivi sasa inaishi kwa msaada wa vyombo vya dola pekee,” alisema Duni akionya kuwa kuwa, hata hivyo, kuiondoa CCM kunahitaji umoja mpana.

“Lakini, ili kazi ya kuiondosha CCM madarakani iwezekane kwa urahisi ni lazima kuwe na mshikamano mpana (grand coalition) wa vyama vyote vya siasa vya upinzani, asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima, wavuvi na wananchi kwa ujumla wake. Hakuna hata mmoja anayeweza kuikabili na kuidondosha CCM peke yake. Sisi ACT-Wazalendo tupo tayari.”

Kupitia kampeni yake mashuhuri ya Shusha Tanga Pandisha Tanga, chama hicho kimeweza kujizolea wanachama wapya zaidi ya 200,000 ndani ya kipindi cha mwezi miezi miwili tu. Hii ni baada ya kiongozi mkuu wa kisiasa visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, kuhamia chama hicho akitokea Chama cha Wananchi (CUF), ambako alifukuzwa uanachama katikati ya mwishoni mwa mwezi Machi 2019.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.