Hivi Tanzania imegeuka pepo ya watekaji?

MIAKA Miwili na Miezi sita tangu Ben Saanane atoweke. Hajulikani alipo. Yu hai au la! Waliohusika na kupotea kwake hawajakamatwa. Hawajulikani. Ni watu wasiojulikana. Ni Story tu!

Mwaka mmoja na miezi sita imepita, tangu mwandishi Azory Gwanda atekwe. Hajulikani alipo. Waliomteka hawajakamatwa. Hawajulikani. Ni watu wasiojulikana. Ni story tu!

Na Luqman Maloto

Mwaka mmoja na miezi 10 imepita tangu aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Simon Kanguye, atekwe. Hajulikani alipo. Waliomteka ni watu wasiojulikana. Upatikanaji wake ni story tu!

Miaka miwili imepita tangu mwanamuziki Roma Mkatoliki na wenzake watatu watekwe kisha kupatikana baada ya siku tatu. Waliowateka ni akina nani? Mpaka leo ni story tu!

Miezi sita imepita tangu mfanyabiashara Mo Dewji alipotekwa. Watekaji walimtelekeza Gymkana, Dar. Akina nani walimteka? Polisi wakatupiga saundi. Mpaka Rais Magufuli akasema “Watanzania siyo wajinga”. Wanaendelea kutusaundisha.

Mamia ya watu wamepotea Kibiti, Mkuranga, Rufiji na Kilwa. Mbunge Bwege alisema bungeni kuwa watu walichukuliwa na polisi lakini vituoni nchi nzima hawapo. Maiti nyingi zikaokotwa Mto Ruvu na fukwe za Bahari ya Hindi. Waliokufa na waliosababisha vifo ni watu wasiojulikana.

Leo tuna story nyingine kuhusu kutekwa kwa kada wa Chadema, maarufu sana mtandaoni kwa jina la “Mdude Chadema”. Alichukuliwa jana na watu wenye bunduki. Hajulikani alipo!

Je, tutapigwa saundi tena kuhusu Mdude? Tanzania ya sasa imekuwa pepo ya watekaji? Maana hawakamatwi? Ni watu wasiojulikana.

Mdude aachiwe haraka akiwa salama. Tudai majibu kuhusu Saanane, Azory, Kanguye na matukio mengine ya utekaji.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.