Congress yamtia hatiani AG Marekani

Kamati ya Sheria ya Bunge la Marekani imepiga kura kumuajibisha Mwanasheria Mkuu William Barr kwa kulidharau bunge hilo kwa kukataa kuwasilisha ripoti kamili kuhusu madai ya uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa mwaka 2016 iliyotayarishwa na mchunguzi maalumu Robert Mueller.

Kamati hiyo yenye idadi kubwa ya wabunge wa chama cha Democratic imeamua kuwa Barr hakulitii bunge. Wabunge 24 wameunga mkono ikilinganishwa na 16 ambao wamekataa na sasa kutapigwa kura nyengine katika Bunge la Wawakilishi ambapo Wademocrat pia ni wengi.

Huku hayo yakijiri ikulu ya White House imezuia kutolewa kwa ripoti hiyo kupitia kwa kifungu cha sheria cha heshima kwa mamlaka.

Hatua hiyo ya White House imeendeleza mzozo wa kikatiba kati ya bunge la wawakilishi linaloongozwa na Wademocrat na Rais Donald Trump kuhusu nguvu yao ya kumchunguza, kuchunguza utawala wake, familia yake na biashara zake.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.