Naibu Spika Venezuela akamatwa

Maafisa wa upelelezi wa Venezuela wamemkamata kiongozi wa ngazi ya juu wa bunge linalotawaliwa na upinzani, Edgar Zambrano, ikiwa ni hatua ya hivi karibuni dhidi ya wabunge walioamua kujiunga na vuguvugu lililoshindikana na kumuondoa madarakani Rais Nicolas Maduro mwezi uliopita.

Zambrano ni naibu wa spika wa Juan Guaido, mtu anayetambuliwa kama kiongozi wa mpito wa Venezuela na mataifa zaidi ya 50, na ambaye aliongoza vuguvugu la kumuondoa madarakani Maduro mnamo Aprili 30.

Rais wa Marekani Donald Trump amelaani hatua hiyo ya kukamatwa kwa Edgar Zambrano. “Kinachotokea nchini Venezuela ni aibu .. Watu wanakufa, hawana chakula, hakuna maji. Hii ni moja ya nchi zilizo tajiri sana ulimwenguni. Na sasa wanaishi vibaya sana. Na tunafanya kazi kwa bidii juu ya tatizo hilo na tunajitahidi kuwa wagumu,” amesema Rais Donald Trump.

Kwa upande mwingine, Mahakama Kuu ya Venezuela iliwashtaki wabunge watatu kuunga mkono uasi wa Guaido uliosababisha siku mbili za mapigano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji.

Chanzo: DW Swahili

Author: Weyani Media

Weyani Media Production (WMP) is a media company which deals with organisation of news stories, exclusive interviews, media events, documentaries, image presentation, photo shooting, video production, special coverages and media media consultancy.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.