Trump aiwekea vikwazo vipya Iran

Marekani imeiwekea Iran vikwazo zaidi kuhusiana na uuzaji wa bidhaa za chuma katika nchi za nje.

Sekta za Iran zilizoathirika na vikwazo hivyo vipya ni sekta ya chuma, chuma cha bati na shaba.

Bidhaa za vyuma vinavyotumika viwandani zinashikilia nafasi ya pili katika bidhaa zinazoiingizia pato kubwa Jamhuri hiyo ya Kiislamu baada ya mafuta.

Rais Trump pia analenga kampuni za kigeni zinazofanya biashara na Iran.

Kulingana na Trump Iran haistahili kukubaliwa tena kufanya biashara ambayo huenda ikapelekea mapato yake kuingia katika mpango wake wa silaha za nyuklia.

Ufaransa imesema inataka njia zake za fedha na Iran zisalie kuwa wazi na kwamba biashara kati yao ni jambo linalowezekana.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.