ANC yakaribia ushindi lakini ushawishi wake waporomoka

Matokeo ya awali kwenye uchaguzi wa Afrika Kusini yamekipa chama tawala cha ANC ushindi wa asillimia 57, mnamo wakati ambapo asilimia 80 ya kura zimeshahisabiwa.

Hata hivyo, chama hicho ambacho kimekuwa madarakani tangu kwa robo karne sasa, kimeshuhudia ushawishi wake ukizidi kupungua.

Matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi, IEC, yanaonesha kuwa chama kikuu cha upinzani, Democratic Alliance, kina asilimia 22 ya kura, huku kile EFF kinachoongozwa na kiongozi wa zamani wa tawi la vijana la ANC, Julius Malema, kikiwa na asilimia 10.

Licha ya ushindi hu, matokeo haya ya uchaguzi wa Jumatano ni mabaya zaidi kwa ANC tangu uchaguzi wa kwanza baada ya utawala wa ubaguzi wa rangi uliomalizika mwaka 1994.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Jumamosi (Mei 11).

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.