England yatoa timu nne Europa League na Champions League

England imekuwa nchi ya kwanza kuwa na timu nne kwenye fainali mbili za mashindano ya Ulaya katika msimu mmoja baada ya Chelsea na Arsenal kutinga katika fainali ya Europa League usiku wa kuamkia leo.

Chelsea iliifunga Eintracht Frankfurt ya Ujerumani mabao 4 – 3 kupitia mikwaju ya penalti uwanjani Stamford Bridge, baada ya kutoka sare ya 1 – 1 kwa mara nyingine tena katika nusu fainali.

Eden Hazard alifunga penalti ya ushindi baada ya mlinda mlango Kepa Arrizabalag kuokoa penalti mbili. Arsenal iliifumua Valencia mabao 4 – 2 huku Pierre-Emerick Aubameyang akifunga mabao matatu ili kukamilisha ushindi wa jumla ya 7-3.

Fainali itachezwa mjini Baku, Azerbaijan mnamo Mei 29.

Timu za England zimetawala soka la Ulaya msimu huu, baada ya Liverpool na Tottenham kufuzu fainali ya Champions League.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.