Mahakama Kuu yaamuru kufutwa vipengele sheria ya uchaguzi Tanzania

Mahakama Kuu nchini Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imesema sheria ya uchaguzi inayowapa uhalali wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi ni batili na hivyo imetamka kuvifuta vipengele viwili katika sheria hiyo.

Katika shauri hilo la katiba lilifunguliwa na mlalamikaji Bob Chache Wangwe, mahakama hiyo imesema baada ya kupokea hoja kutoka pande zote: yaani walamikaji na watetezi ambao ni serikali, imejiridhisha pasina shaka kuwa wakurugenzi hao hawapaswi kuwa sehemu ya usimamizi wa uchaguzi kwa vile hawako huru.

Katika uamuzi wake huo wa leo ambao ulisubiriwa sana na wanaharakati nchini Tanzania, Mahakama hiyo imesema wasimamizi hao ni sehemu ya watendaji wa serikali na kwa vile wao siyo malaika kuna uwezekano mkubwa wakati wakitekeleza majukumu ya usimamizi wa uchaguzi wakaonyesha hali ya upendeleo.

Baada ya hukumu hiyo, wakili wa mlalamikaji, Fatma Karume, alisema uamuzi huo ni ushindi wa kihistoria na hatua moja mbele katika kupigania maslahi ya wapiga kura.

Akiwa ameambatana na kundi la watu wachache, Bob Chache Wange aliyewasilisha hoja hiyo mahakamani, alisema suala la kudai demokrasia ya kweli halipaswi kuwa la mtu mmoja na akawatolewa wito vijana wenzake kudai haki zao pasina woga.

Bado serikali haijaweka bayana kama itaikatia rufaa hukumu hiyo au la. Tanzania mwaka huu inatarajiwa kuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa na baadaye mwakani kukifanyika uchaguzi mkuu.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.