Mbunge mwengine Venezuela aomba hifadhi ubalozini

Italia imethibitisha kuwa mwanasiasa wa Venezuela mwenye asili ya Italia, Americo De Grazia, ameomba hifadhi kwenye makaazi ya balozi wa Italia mjini Caracas.

De Grazia, ambaye ni mbunge wa upinzani nchini Venezuela, amekuwa mwanasiasa wa hivi karibuni kabisa kukimbia balozi za kigeni, baada ya msako unaofanywa na vikosi vya Rais Nicolas Maduro.

Wizara ya mambo ya nje ya Italia imesema kuwa imemkaribisha mwanasiasa huyo na kwamba haijakiuka kanuni za kidiplomasia. Juzi Jumatano, naibu spika wa bunge linalodhibitiwa na upinzani nchini Venezuela, Edgar Zambrano, alikamatwa.

Kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kaimu rais Juan Guaido amesema kukamatwa huko kuna maana sasa wabunge wanalengwa ikiwa ni ishara ya serikali kukata tamaa na ambayo viongozi wake hawajui ni nani watakayemuamini.

Kiongozi huyo wa upinzani anayeungwa mkono na Marekani ametangaza maandamano ya kitaifa Jumamosi, baada ya makabiliano ya wiki iliyopita kusababisha vifo vya watu sita.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.