Watu wenye silaha wavamia hoteli Pakistan

Watu wenye silaha wameivamia hoteli moja nchini Pakistan katika mji wa bandari wa Gwadar na kumuua mlinzi mmoja.

Katika tukio hilo, wavamizi watatu walimuua kwa risasi mlinzi huyo aliyekuwa katika lango la hoteli hiyo inayotumiwa zaidi na wawekezaji wa kigeni ambao hawakuwepo katika eneo hilo wakati wa uvamizi huo.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Ziaullah Langove, amesema wageni wengi waliondolewa kutoka katika hoteli hiyo ya nyota tano ya Pearl Continent, ambayo ilikuwa imezingirwa na helikopta wakati mapigano yakiendelea.

Polisi wamethibitisha kuwa watu wawili wamejeruhiwa katika tukio hilo ingawa huenda kukawa na majeruhi wengine.

Kundi la Balochistan Liberation Army la nchini humo limekiri kuhusika na tukio hilo likisema liliwalenga raia wa China na wawekezaji wa kigeni na kwamba lengo lao limetimia.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.