Omar al-Bashir ashitakiwa kwa mauaji ya waandamanaji

Rais wa zamani wa Sudan amefunguliwa mashitaka juu ya kuuliwa kwa waandamanaji wakati wa maandamano ya kuipinga serikali ambayo yalipelekea kuondoshwa kwake madarakani.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo Jumatatu (Mei 14), ofisi ya kaimu mwendesha mashitaka mkuu wa Sudan imesema kuwa “Omar al-Bashir na wenziwe wameshitakiwa kwa kuchochea na kushiriki kwenye mauaji dhidi ya waandamanaji.”

Mapema mwezi huu, mwendesha mashitaka aliamuru al-Bashir ahojiwe kutokana na tuhuma za kutakatisha fedha na kufadhili ugaidi.

Hakujapatikana kauli yoyote kutoka kwa rais huyo wa zamani tangu aondolewe madarakani na kukamatwa hapo tarehe 11 Aprili.

Tangazo hili la mashitaka lilikuja siku ambayo waandamanaji na baraza la kijeshi lilianza tena mazungumzo ya kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Chanzo: Al Jazeera English

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.