Trump Jr. kuhojiwa na bunge Marekani

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa mwanawe Rais wa Marekani Donald Trump, Donald Trump Junior, amefikia makubaliano na kamati ya ujasusi ya baraza la senate la Marekani kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano na jopo la kamati hiyo katikati ya mwezi Juni.

Likimnukuu mtu ambaye alifahamishwa kuhusiana na makubaliano hayo, gazeti hilo limesema kikao hicho cha faragha kitajumuisha maswali kuhusu mada sita na kitadumu kwa chini ya saa nne.

Kamati hiyo ya seneti inayoongozwa na wabunge wa chama cha Republican ilikuwa imemuita Donald Trump Junior wiki iliyopita kuhudhuria kikao hicho ili ajibu maswali kuhusiana na maafisa wa Urusi aliowasiliana nao.

Ushahidi wa kwanza alioutoa Trump Junior mbele ya kamati hiyo ulikuwa kuhusu ushiriki wake katika mkutano wa mwezi Juni mwaka 2016 katika jengo la Trump Tower ambapo alikutana na raia wa Urusi waliompa taarifa kuhusu mgombea wa urais wa chama cha Democratic wakati huo, Hillary Clinton, aliyekuwa anashindana na Donald Trump.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.