Muungano wa vyama tawala washinda Australia

Kiongozi wa upinzani nchini Australia, Bill Shorten, amekubali kushindwa na Waziri Mkuu Scott Morrison katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo.

Shorten alitoa tangazo mbele ya wafuasi wa chama cha upinzani cha Labor masaa machache baada ya matokeo ya uchaguzi kuonesha kuwa chama chake kilikuwa kimeshindwa kupata wingi wa kura kuweza kuunda serikali.

Kabla ya tangazo hilo, mwanasiasa huyo alimpigia simu Waziri Mkuu Morrison kumpongeza kwa ushindi ambao chama chake kimeupata.

Televisheni ya taifa ilitangaza kuwa muungano unaongozwa na chama cha kihafidhina cha Waziri Mkuu Morrison umepata viti 74 katika bunge lenye viti 151 na wakati chama cha Shorten kimeambulia viti 65.

Jumla ya viti 74 vinahitajika kwa chama kuweza kuunda serikali nchini Australia.

Chanzo: DW Swahili

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.