Naibu Kansela ajiuzulu kwa ufisadi

Naibu Kansela wa Austria, Heinz-Christian Strache, amejiuzulu baada ya kuchapishwa vidio ya siri iliyomuonesha akitoa mikataba ya serikali ili kupata uungwaji mkono wa kisiasa.

Strache amesema amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa Kansela Sebastian Kurz mapema leo (18 Mei)  ili kuzuia kuanguka kwa muungano unaotawala nchini Austria kati ya chama cha kihafidhina cha Kansela Kurz na na kile cha cha mrengo mkali wa kulia cha Naibu huyo.

Ingawa amesisitiza kuwa hakuvunja sheria yoyote, Strache amekiri juu ya mahusiano ya kuaibisha ambayo yalimuonesha akitoa mikataba ya ujenzi wa miundombinu kwa mwanamke mmoja tajiri kutoka Urusi.

Mazungumzo katika ukanda huo wa vidio uliotolewa na magazeti ya Der Spiegel na Sueddeutsche Zeitung yalifanyika katika kisiwa cha Ibiza nchini Uhispania mwaka 2017, miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa bunge uliokiingiza madarakani chama cha Strach.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.