Kansela wa Austria kumfuta kazi waziri wa mambo ya ndani

Kuna dalili zinazoashiria kuwa Kansela Sebastian Kurz wa Austria anajiandaa kumfuta kazi waziri wa mambo ya ndani, anayetoka katika chama cha sera kali za mrengo wa kulia cha FPÖ kinachokumbwa na kashfa.

Kashfa hiyo iliibuka baada ya kufichuliwa mkanda wa video unaomwonyesha kiongozi wa chama hicho, Heinz-Christian Strache, ambaye alikuwa naibu kansela, akizungumza na wakala wa tajiri kutoka Urusi, kuhusu njama za kumpendelea katika zabuni za serikali na kukiuka taratibu za kifedha.

Strache alijiuzulu wadhifa wake kutokana na kashfa hiyo. Waziri kutoka chama cha Kansela Kurz, Gernot Bluemel amekiambia kituo cha televisheni cha ORF kwamba kansela huyo atamfuta kazi Herbert Kickl, waziri wa mambo ya ndani ambaye ana ushawishi mkubwa katika chama cha FPÖ.

Bluemel amesema hatua hiyo itakuwa na malengo ya kuhitimisha kashfa hiyo iliyomlazimisha Kansela Kurz kuitisha uchaguzi wa mapema.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.