Trump atishia kuimaliza Iran

Rais Donald Trump wa Marekani ameionya Iran kutothubutu tena kuitishia Marekani, la sivyo itatokomezwa rasmi.

Onyo la Trump lililotolewa kupitia mtandao wa Twitter, limekuja muda mfupi baada ya roketi kuanguka karibu na ubalozi wa Marekani mjini Baghdad, Iraq, usiku wa kuamkia leo.

Hakuna kundi lolote lililodai kulirusha roketi hilo.

Haya yanajiri wakati mvutano baina ya Marekani na Iran ukifika katika kiwango cha juu kabisa.

Mvutano huo ulishika kasi mwaka jana baada ya Trump kuiondoa Marekani katika makubaliano juu ya mpango wa nyuklia wa Iran, ambao ulifikiwa kati ya Iran ya mataifa makubwa duniani.

Trump ameandika kuwa ikiwa Iran inataka vita, huo utakuwa mwisho wake.

Hakutoa maelezo kuhusu kitisho chake hicho, na wala Ikulu ya White House haikufafanua zaidi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.