Marekani yamfungulia mashtaka mapya Assange

Marekani imemfungilia mashitaka mapya muasisi wa tovuti ya uvujishaji wa nyaraka za siri Wikileaks, Julian Assange, ikimtuhumu kwa kuiweka Marekani katika kitisho cha kukumbwa na “madhara makubwa” kwa kuchapisha nyaraka mnamo mwaka wa 2010.

Mashitaka hayo 17 yaliyowasilishwa na waendesha mashitaka wa Wizara ya Sheria yanadai kuwa Assange alisaidia katika wizi wa nyaraka za siri, na akazichapisha hovyo taarifa za siri.

Muasisi huyo wa Wikileaks sasa anakabiliwa na jumla ya mashitaka 18 ya uhalifu, na huenda akakabiliwa na adhabu ya kutupwa gerezani kwa miongo mingi kama atahamishwa kutoka Uingereza na kuhukumiwa nchini Marekani.

Waendesha mashitaka wanamtuhumu Assange kwa kumuagiza aliyekuwa mtaalamu wa ujasusi wa jeshi la Marekani Chelsea Manning kutafuta na kisha kuvujisha taarifa za siri zenye kusababisha uharibifu mkubwa.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.