Ethiopia: Mkuu wa Jeshi apigwa risasi

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amefahamisha kuwa mkuu wa majeshi Seare Mekonen alipigwa risasi baada ya kuzuka machafuko Jumamosi jioni katika taifa hilo la Pembe ya Afrika. Hata hivyo hali ya mkuu huyo wa jeshi haijulikani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa shirika la habari la AFP, Abiy alizungumza kupitia kwenye televisheni ya taifa akiwa amevaa mavazi rasmi ya kijeshi baada ya kutokea jaribio la mapinduzi katika jimbo la Amhara lakini maelezo zaidi hayakutolewa kuhusiana na lengo la mashambulio hayo katika jimbo la pili lenye watu wengi zaidi nchini Ethiopia linaloongozwa na rais wa kikanda Ambachew Mekonen.

Ubalozi wa Marekani ulitoa tahadhari baada ya kusisikia milio ya bunduki katika mji mkuu wa Addis Ababa, na pia vurugu karibu na mji mkuu wa jimbo la Amhara, Bahir Dar.

Serikali ya Ethiopia imesema jaribio hilo la kuipindua serikali ya kikanda kaskazini mwa nchi hiyo lilishindikana. Ofisi ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imelaani jaribio hilo la mapinduzi katika ujumbe wa Twitter uliochapishwa Jumamosi jioni.

Chanzo: DW Kiswahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.