Itumbi ahojiwa barua ya kumuua Naibu Rais Ruto

Aliyekuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya kidijitali katika ikulu nchini Kenya, Dennis Itumbi, amezuiwa na polisi kuhojiwa kuhusu barua ya njama ya kumuua Naibu Rais William Ruto.

Itumbi amekamatwa na wapelelezi wanaochunguza tuhuma za njama ya kumuua Naibu Rais Ruto.

Anazuiwa katika makao makuu ya idara ya upelelezi mjini Nairobi, linaripoti gazeti la The Standard.

Anakamatwa siku kadhaa baada ya taarifa kwamba chanzo cha barua hiyo ghushi kimetambulika – barua iliyozusha tuhuma za kutaka kuuawa Ruto.Ruka ujumbe wa Twitter wa @BreakingNewsKEView image on Twitter

View image on Twitter

CapitalFM Breaking News@BreakingNewsKE

DENNIS Itumbi arrested for questioning by DCI officers in probe over fake letter on DP Ruto assassination claims.523:33 AM – Jul 3, 201926 people are talking about thisTwitter Ads info and privacy

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @BreakingNewsKE

Wiki iliyopita, mawaziri kadhaa nchini Kenya walikana kupanga njama za kumuua Naibu Rais William Ruto.

Waziri wa biashara wa Kenya Peter Munya amekana shutuma za kupanga mauaji ya Naibu Rais William Ruto, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Waziri Munya alikuwa akizungumza nje ya makao makuu ya ofisi ya Mkurugenzi wa uchunguzi wa makosa ya jinai (DCI) ambako aliitwa , sambamba na mawaziri wengine, kuhojiwa kuhusu shutuma kuwa walimtishia bwana Ruto, gazeti la The Standard limeripoti.Ruka ujumbe wa Twitter wa @K24Tv

K24 TV@K24Tv

BREAKING: Dennis Itumbi ARRESTED! https://www.k24tv.co.ke/news/dennis-itumbi-arrested-1902/ …513:32 AM – Jul 3, 2019Twitter Ads info and privacyDennis Itumbi arrested – K24 TVBlogger-turned-Jubilee digital strategist, Dennis Itumbi, has been arrested.k24tv.co.ke21 people are talking about this

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @K24Tv

Wameshutumiwa kufanya vikao vya siri, The Standard limeongeza, lakini bwana Munya amewaambia waandishi wa habari kuwa hawajapeleka taarifa polisi kwa kuwa bwana Ruto hajapeleka malalamiko rasmi.

Daily Nation la Kenya lilimnukuu waziri akisema kuwa Naibu Rais Ruto alidai kuwa mawaziri hao walikuwa wakifanya vikao vya siri na maafisa wengine.

Naibu Rais Ruto ana mipango ya kuwania urais mwaka 2022.

Chanzo: BBC Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.