Mberesero na wenziwe wahukumiwa kwa ugaidi Garissa

Mahakama moja mjini Nairobi imewahukumu washukiwa watatu wa ugaidi nchini Kenya waliopatikana na hatia ya kufanya shambulio la mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa.

Rashid Charles Mberesero, raia wa Tanzania anayetuhumiwa kuhusika katika shambulio hilo amehukumiwa maisha gerezani

Wengine wawili Hassan Edin na Mohammed Abdi jina jingine Mohamned Ali Abikar wamehukumiwa miaka 41 kila mmoja gerezani.

Wote walipatikana na hatia ya kupanga shambulio hilo chini ya ushirikiano wa wanachama wa kundi la Al-Shabab.

Takriban wanafunzi 148 walifariki katika shambulio hilo.

Kadhalika hukumu hiyo imepitishwa baada ya watatu hao kupatikana na hatia ya kuwa wanachama wa kundi la al-Shabaab kutoka Somalia.

Mwezi uliopita, mahakama nchini Kenya ilimuachilia huru Sahal Diriye Hussein aliyetuhumiwa kufanya shambulio la 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa lililosababisha vifo vya takfriban watu 150.

Awali kesi hiyo ilichelewa kuanza leo mchana baada ya wakili wa mmojawapo wa watuhumiwa Rashid Charles Mbeserero, raia wa Tanzania kushindwa kutokea mahakamani.

Hatua iliyosababisha Jaji Francis Andayi kutoa agizo kwa mawakili na kusukuma mbele kusomwa hukumu hiyo.

Chanzo: BBC Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.