Zaidi ya raia 100 wauawa Sudan Kusini katika machafuko mapya – UN

Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa mzozo umeongezeka katika eneo moja la Sudan Kusini tangu makubaliano ya amani yaliposainiwa.

Na kwamba mamia ya raia wamenajisiwa au wameuawa na pande hasimu kwenye machafuko hayo. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNIMISS, umesema raia wamelengwa na kuvamiwa kimakusudi katika jimbo la Central Equatoria, tangu mkataba uliosainiwa Septemba mwaka uliopita.

Ujumbe huo umesema kuwa watu wasiopungua 104 wameuawa kwenye mashambulizi katika vijiji vya jimbo hilo la kusini mwa nchi hiyo. Katika ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu haki za binaadamu, ujumbe huo umeongeza kuwa takriban idadi sawa na hiyo ya wasichana na wanawake pia walinajisiwa au walidhulumiwa kingono kati ya mwezi Septemba mwaka jana hadi Aprili mwaka huu.

Ongezeko la machafuko nchini humo limesababisha zaidi ya watu 56,000 kukimbia makwao na kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao, huku wengine 20,000 wakikimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.