China yaitaka Uingereza kukoma kuingilia masuala ya ndani ya Hong Kong

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt, ameahidi kuendelea kuishinikiza China kuhusu njia za nguvu inazotumia dhidi ya waandamanaji mjini Hong Kong huku mzozo wa kidplomasia ukiongezeka.

Hunt amerejelea kuwa kutakuwa na athari iwapo China itakiuka makubaliano yalioafikwa kuhusu haki mjini Hong Kong wakati Uingereza ilipoikabidhi uthibiti.

Akizungumza na BBC radio , Hunt alikataa kutaja hatua maalum zitakazochukuliwa lakini akasema kuwa hatua hizo zinapaswa kuachwa wazi   na kwamba kile alichotaka kufanya ni kuweka ujumbe wazi kuwa hili sio jambo ambalo litapuuzwa na kuendelea mbele  lakini litakuwa suala muhimu sana kwa Uingereza.

Baada ya onyo la kwanza la Hunt siku ya jumanne la kuchukuwa hatua dhidi ya China , wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya China imejibu kwa kumshtumu Hunt kwa kujiingiza katika nadharia za kikoloni.

Balozi wa China nchini  Uingereza Liu Xiaoming hapo jana alizungumza na waandishi habari  na kuitaka Uingereza kukoma kuingilia masuala ya ndani ya Hong Kong.

Balozi huyo pia ameonya kuwa hatua hiyo inatishia kuendelea kuharibu uhusiano kati ya mataifa hayo mawili .

Liu Xiaoming baadaye alitakiwa kufika katika wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Uingereza mjini London.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.