Marekani na Taliban waandika upya mswada wa kuondoa majeshi

Wajumbe wa majadiliano wa Taliban na Marekani wanakwenda mbio kuandika upya mswada wa makubaliano yatakayoainisha kuondoka majeshi ya Marekani na NATO kutoka Afghanistan na uhakikisho wa Taliban kupinga ugaidi.

Matukio ya Kisiasa

Marekani na Taliban waandika upya mswada wa kuondoa majeshi

Wajumbe wa majadiliano wa Taliban na Marekani wanakwenda mbio kuandika upya mswada wa makubaliano yatakayoainisha kuondoka  majeshi ya Marekani na NATO kutoka  Afghanistan na uhakikisho wa Taliban kupinga ugaidi.

Makubaliano hayo  pia  ni  pamoja  na  kupata  uhakikisho  madhubuti wa  Taliban  wa kupambana  na  ugaidi kabla  ya  mkutano wa  amani kwa  ajili  ya makundi  yote  ya  Afghanistan  utakaofanyika  siku  ya Jumapili. 

Maafisa  ambao  wako  karibu  na  majadiliano  hayo, lakini  ambao hawana  mamlaka  ya  kuyazungumzia , wanasema  majadiliano yameingia  katika  nyakati  za  usiku  jana  Jumatano na  wajumbe watarejea  tena  leo  Alhamis  katika  mazungumzo,  hayo  ya  ana kwa  ana  ambayo  yamechukua  siku  sita   kati  ya  wapiganaji hao na  mjumbe  wa  Marekani Zalmay Khalilzad.

Suhail Shaheen, msemaji wa  ofisi  ya  kisiasa  ya  Taliban nchini Qatar, mapema  aliliambia  shirika  la  habari  la  Associated Press kwamba  mswada  wa  makubaliano  unaandikwa  upya  kujumuisha vipengee  vilivyokubaliwa  kwa  pamoja. Pande  hizo  mbili  bado zimegawika  kuhusiana  na  muda wa  kuyaondoa  majeshi, wakati Marekani  inataka  muda  zaidi.

Maafisa  wa  Taliban , ambao  walizungumza  kwa  masharti  ya kutotajwa   majina, wamesema  Marekani  inataka  miezi 18 kukamilisha  kuviondoa  vikosi  vyake vyote  hata  kama  Rais  wa Marekani  Donald Trump  amekiambia  kituo  cha  televisheni  cha Fox News  mapema  wiki  hii  kuwa  uondoaji  wa  vikosi  tayari umeanza  kimya  kimya  na  kwamba nguvu  za  vikosi  hivyo imepunguzwa  hadi  wanajeshi 9,000.

Taarifa  ya  Rais  Trump imekuwa  tangu  wakati  huo  ikikinzana  na  taarifa  za maafisa waandamizi  wa  Marekani,  ambao  wamesema  nguvu  ya  majeshi hayo  haijabadilika  na  iko  katika  jumla  ya  wanajeshi 14,000.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.