Mtihani wa mwisho India: Utata uliosababisha vifo vya wanafunzi 23

Takriban vijana 23 katika jimbo la kusini mwa India la Telangana wamejitoa uhai tangu matokeo ya mtihani wao yatangazwe mnamo mwezi Aprili. Mwandishi wa BBC wa Telugu Deepthi Bathini anaelezea jinsi matokeo hayo yalivyokumbwa na utata

Thota Vennela alifurahia sana kupika, kutazama vipindi vya vichekesho na kula chakula kinachouzwa barabarani.

Nduguye mkubwa , kwa jina Venkatesh ,19, hivi majuzi alimfunza kupeleka baiskeli .

”Nilifurahi sana kwamba alikuwa anaweza kupeleka baiskeli hiyo kama mtaalam. Lakini mara nyengine nilimfuata bila yeye kujua ili kuhakikisha kuwa yuko salama”, amnasema.

Vijana hao walizozana kuhusu baiskeli hiyo lakini walikuwa marafiki sana.

Venkatesha anashindwa kuzuia machozi yake anapotoa kipochi chake ili kuonyesha picha ya dada yake. Mnamo tarehe 18 mwezi Aprili – siku aliyogundua kwamba amefeli katika darasa lake la 12 Vennela alikula sumu. Alifariki saa chache hospitalini.

Vennela nduguye Venkatesh
Image captionVennela na nduguye Venkatesh walikuwa wakipendana sana

Alirudia mara kwa mara ‘niliweza vipi kufeli’? Anakumbuka mamake, Sunitha. ”Tulimbembeleza na kumwambia kwamba ni sawa na kwamba angewasilisha ombi jingine kufanya tena mtihani huo. Lakini hata alipokuwa hospitalini aliendelea kusema ‘ningepita mtihani’.

Vennela alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi 320,000 wa Telangana waliofeli mtihani wao. Wote walipelekwa katika shule ambayo inafunza mtaala uliobuniwa na bodi ya elimu ya serikali.

Elimu ya juu nchini India hukabiliwa na ushindani mkali.

Hivyoibasi mitihani ya mwisho katika shule huwa muhimu sana kwa kuwa itakusaidia kujiunga na vyuo vikuu vizuri – ambavyo huonekana kama tiketi za ajira nzuri zenye mapato ya juu na maisha mazuri.

Vyuo vikuu pia hufanya mitihani huru , lakini wanafunzi ambao hupata matokeo mazuri katika mtihani huo mara nyengine hukosa kuendelea na masomo iwapo watafeli mtihani wa mwisho.

Siku chache baada ya matokeo hayo kutangazwa wanafunzi walioshangazwa na matokeo pamoja na wazazi waliandamana, wakidai kwamba kulikuwa na makosa katika usahihishaji wa mtihani huo na kutaka mtihani huo kusahihishwa kwa mara ya pili.

Venugopal Reddy
Image captionVenugopal Reddy anasema ana wasiwasi kuhuu mwanawe

“Mwanangu alipata matokeo mazuri katika somo la hesabati, fizikia , kemistry katika mtihani wa darasa lake la 11. Lakini mwaka huu matokeo yanaonyesha kwamba alipata alama moja katika somo la hesabati na sufuri katika somo la Fizikia. Hilo linawezekanaje”?, alisema Venugopal Reddy.

Amekuwa akisomea mitihani mingine yenye ushindani mkali . Lakini baada ya matokeo amekatika tamaa. Amewacha kusoma na kula na anakataa kutoka nyumbani .

”Nina wasiwasi kuhusu afya yake ya akili” , anaongezea.

Na huku maandamano hayo yakishika kasi, visa vya wanafunzi waliofeli mtihani huo kujiua viliongezeka katika maeneo mbali mbali ya jimbo hilo.

Kundi moja la wanaharakati wa haki za kibinadamu liliwasilisha malalamishi katika mahakama kuu , ambayo yaliagiza bodi hiyo kusahihisha tena matokeo yote ya wanafunzi waliofeli katika jimbo hilo.

Matokeo mapya yalitangazwa tarehe 27 mwezi Mei – ambapo matokeo ya wanafunzi 1,137 waliofeli yaliangaziwa upya na ikabainika kwamba walikuwa wamefanikiwa.

Mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa amepata sufuri katika somo moja alipata alama 99 wakati makaratasi yake yaliposahihishwa tena.Intense competition for a prestigious degree is fuelling demand in India’s private coaching industry.

Katikati ya utata huo ni kampuni moja ya kibinafasi ya teknolojia Globarena Technology, ambayo 2017 ilishinda kandarasi ya serikali kuendesha mtihani huo katika jimbo hilo lenye wanafunzi 970,000.

Pia kampuni hiyo ilikuwa ikihusika na kusahihisha matokeo ya mtihani huo kabla ya kutangazwa.

Bodi ya serikali inayobuni mitihani , ambayo ilitoa kandarasi ya mitihani kwa kampuni ya Globarena imesema kuwa visa vya kujitoa uhai havihusiki kamwe na makosa ya usahihishaji wa mitihani hiyo.

Globarena ilikiri kwamba kulikuwa na makosa.

”Tunafuata mchakato uliotolewa na bodi. Visa vilivyotokea havikutarajiwa . Ni kweli kulikuwa na makosa awali lakini sasa tumefanya marekebisho, VSN Raju afisa mtendakazi a kampuni hiyo aliambia BBC mwezi Aprili.

Anamika Yadav
Image captionAnamika alitakabkujiunga na jeshi la India

Familia ya mwanafunzi mmoja aliyejiuwa – Anamika Yadav imesema kwamba atawasilisha mashtaka ya uhalifu dhidi ya bodi ya elimu na kampuni ya Globarena.

Familia yake iliambia BBC kwamba kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 alijiuwa baada ya kubaini kwamba amefeli mtihani wake wa mwisho .

Tarehe 27 mwezi Mei, waliosahihisha mtihani wake kwa mara ya pili waliutangaza kwamba amepita mtihani huo, lakini saa chache baadaye-matokeo hayo yalibadilishwa na kuambiwa kwamba alifeli tena.

Inaonekana kwamba kulikuwa na makosa katika kubadilisha matokeo hayo .

Maafisa wa bodi walisema kuwa Globarena haikuhusishwa katika mchakato wa kusahihisha upya.

”Hiki ni kitendo kinacholeta shauku” , alisema babake Anamika, Atul Ganesh.

Babake Vennela Gopalakrishna , pia anataka kuwasilisha mashtaka mahakamani.

”Siwezi kuiamini bodi. Ni vipi mwanangu ambaye ni mwanafunzi mzuri” , anafeli? ”Nahitaji majibu”.

Familia ya Shivani imeweka bango la kumbukumbu yake

Usahihishaji huo haukutoa majibu ya wanafunzi waliojitoa uhai. Lakini wazazi wao hawajui cha kufanya na matokeo hayo -wameshangazwa na kuvunjika moyo, mbali na kwamba wamejaa wasiwasi mwingi.

Wazazi wengi walizungumzi ari waliokuwa nayo wana wao. Vodnali Shivani ,16, alikuwa akiamka mapema alifajiri ili kusoma.

Alitaka kuwa muhandisi na mara kwa mara angesikika akimwambia babake: Subiri kwa miaka mitano na maisha yetu yatabadilika.

Devasothu Neerja alitaka kuwa daktari, na alitumia wakati wake mwingi wa usiku akisoma.

Alikuwa akipita mitihani yake yote. Hivyobasi tulifikiria kwamba tunafaa kutumia kila mbinu kumsaidia, alisema babake, Rupal Singh.

chanzo: bbc

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.