Zanzibar: Injinia wa Meli ajinyonga safarini

Mtu mmoja anayetajwa kuwa Injinia wa Meli ya MV Mapinduzi inayofanya safari zake Unguja na Pemba, Haji Abdallah Khatib, amejinyonga wakati Meli hiyo ikiwa safarini kutoka Unguja kwenda Pemba.

Meli ya MV Mapinduzi

Mkurugenzi wa Shirika la Meli na  Uwakala Zanzibar Salum Ahmada Vuai, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo ameeleza kuwa mtu huyo alikuwa kwenye chumba cha mashine na alikuwa peke yake.

”NI kweli amejinyonga lakini ni mapema sana kujua chanzo lakini Meli imelazimika kukatisha safari yake na kurejea Unguja kwaajili ya uchunguzi zaidi”, amesema Vuai.

Awali Kamanda wa Polisi wa Mjini Magharibi Thobias Sedeyoka, aliiambia EATV&EA Radio Digital kuwa athari ya tukio hilo inakwenda kwa abiria wengine ambao leo ni siku ya kwanza ya wiki na walikuwa wanakwenda kwenye majukumu yao lakini wanalazimika kurudi.

”Bado tunaongea na mamlaka husika ili kujua lakini tu kama mnavyofahamu leo ni Jumatatu watu wanakwenda kwenye shughuli zao huo Pemba lakini sasa wanarudi Unguja ili tuupate mwili na tufanye uchunguzi kisha tutawajulisha zaidi”, ameeleza.

vyanzo: EATV&EA Radio Digital

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.