Bale, Pogba, Lo Celso, Sessegnon, Alderweireld, Rose, Rodriguez, Messi

Uwezekano wa Real Madrid kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba, 26, utategemea kuondoka kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 30, kuondoka klabu hiyo ya Uhispania. (AS)

Bale, ambaye anapokea pauni 550,000 kwa wiki katika uga wa Bernabeu, ambako ana mkataba wa hadi mwaka 2022, anataka marupu rupu yanayolingana na wachezaji wakuu duniani kuondoka Real Madrid, kinasema chanzo cha habari kilicho na uhusiano wa karibu na nyota huyo. (Sky Sports)

Barcelona wako tayari kufanya mazungumzo na Lionel Messi, 32, kurefusha mkataba wa nyota huyo raia wa Argentina kwa miaka minne zaidi. (ESPN)

Lionel Messi
Image captionLionel Messi ameshinda mataji manne ya Ulaya

Tottenham wanajiandaa kutumia tena kitita kikubwa cha fedha wiki hii kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Real Betis na Argentina Giovani lo Celso, 23, pamoja na mlinzi wa wa chini ya miaka 21 wa Fulham na England, Ryan Sessegnon, 19. (Mirror)

Giovani Lo Celso aliifungia Real Betis mabao 16 msimu uliopita
Image captionGiovani Lo Celso aliifungia Real Betis mabao 16 msimu uliopita

Fulham wanataka pauni milioni 40 kumuachilia Sessegnon lakini Spurs wanamini wanaweza kuafikiana kwa mkataba wa karibu pauni milioni 25 kumnasa mchezaji huyo ambaye amesalia na mwaka mmoja kukamilisha mkataba wake Craven Cottage.

Sessegnon pia anapania kusalia London, japo vilabu vingine vikubwa kama vile Manchester United, Paris St-Germain, Juventus na Borussia Dortmund pia vimekuwa vikimfuatilia. (London Evening Standard)

Kiungo wa Fulham Ryan Sessegnon (kulia) akimkaba mlinzi wa Southampton Jack Stephens
Image captionRyan Sessegnon (kulia)

Toby Alderweireld anatarajia kubaka Tottenham, licha ya Roma kuhusishwa na uhamisho wa mlinzi huyo wa miaka 30 raia wa Ubelgiji ambaye masharti ya mkataba wake yanasema lazima auzwe ikiwa klabu inayotaka kumnunua ina uwezo wa kufikia ada ya pauni milioni 25 kufikia Alhamisi wiki hii. (Telegraph)

Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri anataka kumjumuisha mlinzi wa Tottenham Danny Rose, 29, katika kikosi chake cha Juventus. (Mail)

Danny Rose
Image captionDanny Rose

Atletico Madrid huenda wakaelekeza juhudi zao katika harakati ya kumsaka mchezaji nyota wa Real Madrid MColombia James Rodriguez, 28, badala ya kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27. (Marca)

Antoine Griezmann, 28, ameashiria kuna ”uwezekano” wa kujiunga na Manchester United siku zijazo huku mchezaji huyo mpya wa Barcelona akielezea azma yake ya kucheza na mchezaji mwenza wa Ufaransa na mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 28, katika soka ya kiwango cha vilabu. (Goal.com)

Antoine Griezmann
Image captionAntoine Griezmann

Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, anajiandaa kutia saini mkataba ulioboreshwa wa thamani ya pauni milioni 117 ambao huenda ukaendelea hadi mwaka 2025, na pia anataka kuwa nahodha Old Trafford. (Manchester Evening News)

Mlinzi wa England Harry Maguire, 26, hana mpango wa kuhama Leicester licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa Manchester United. (Leicester Mercury)

Harry Maguire
Image captionHarry Maguire

Juventus wako tayari kuizia Manchester United mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, msimu huu wa joto, bei yao ya kati ya £70m na pauni milioni 90 ikifikiwa. (Mail)

Mshambuliaji wa zamani wa Crystal Palace Clinton Morrison anatarajia mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, atasalia katika uwanja wa Selhurst Park msimu huu, licha ya mchezaji huyo kunyatiwa na Arsenal Bayern Munich. (Talksport)

Wilfried Zaha
Image captionZaha aliifungia Palce mabao 10 katika msimu wa mwaka 2018-19

Arsenal wako mbali sana kufikia kiwango cha pauni milioni 80 zinazoitishwa na Crystal Palace kumwachilia Zaha, huku wasimamizi wa Selhurst Park wakipuuzilia mbali ofa za hivi karibuni za kutaka kumnunua kiungo huyo. (Independent)

Wolves wako tayari kuweka dau la pili la kumnunu a mlinzi wa Olympiacos Pape Abou Cisse, 23. (Sport Witness, via Birmingham Mail)

Kiungo wa kati wa Brighton Taylor Richards, 18, anasema haikuwa rahisi kufanya uamuzi wa kuondoka Manchester City kwenda Seagulls. (Argus)

Tetesi Bora Jumatatu

Klabu ya ligi ya Uchina Beijing Guoan wamepania kumsajili winga wa Real Madrid Gareth Bale. Klabu hiyo, ina mpango wa kumfanya winga huyo mwenye miaka 30 kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi ya Uchina. (telegraph)

Real Madrid

Manchester United, ambao awali walikuwa wakimnyemelea Bale wamejitoa katika mbio za kumsajili mchezaji huyo. (Manchester Evening News).

Beki wa Arsenal na Ufaransa Laurent Kolscielny amekubali kujiunga na klabu ya Rennes. (RMC Sport).

Arsenal inatarajiwa kuishinda Tottenham katika kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos. Mchezaji huyo wa Uhispania atajiunga kwa mkopo.(Mirror)

Kiungo wa kati wa Liverpool na Uingereza James Milner ,33, amesema hajui hatma yake katika klabu hiyo licha ya kwamba anataka kusalia. (Liverpool Echo)

chanzo:bbc

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.