Boris Johnson kuteuliwa Waziri Mkuu mpya Uingereza

Boris Johnson amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama cha Conservative katika kura iliyopigwa na wanachama na atakuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza.

Amemshinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa kura 92,153 dhidi ya 46,656.

Meya huyo wa zamani wa mji wa Londona anapokea wadhifa huo kutoka kwa Theresa May kesho Jumatano.

Katika hotuba yake baada ya ushindi huo, Johnson ameahidi kuwa “ataiwasilisha Brexit, kuiunganisha nchi na kumshinda Jeremy Corbyn”.

Akizungumza mjini London, alisema: “Tutaipa nchi nguvu.

Tory leadership result

“Tutaiwasilisha Brexit kufikia Oktoba 31 na kuchukua fursa zote zitakazotokana na muamko mpya wa inawezekana.

“Tutajiamini upya na tutainuka upya na kuondosha shaka na fikra za kutojiamini.”

Takriban wanachama 160,000 wa Conservative walikuwa na fursa ya kupiga kura na katika waliojitokeza ni 87.4%.

Asilimia ya kura kwa Johnson – 66.4% – ilikuwa chini ya aliyojishindia waziri mkuu wa zamani David Cameron mnamo mwaka 2005 aliyejinyakulia 67.6%.

Ushindi umepokewaje?

Bi May amempongeza Johnson, na kumauhidi “ushirikiano wake kikamilifu kutoka nafasi ya nyuma”.

Rais wa Marekani Donald Trump pia ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter akimpongeza Johnson, na kuongeza: “Atakuwa mzuri mno!”

Jeremy Corbyn ralituma ujumbe kwenye twitter kwamba “ameshinda uungwaji mkono wanachama chini ya 100, 000 wasiowakilisha wa chama cha Conservative”, lakini “hajashinda uungwaji mkono wa nchi yetu”.

Trump on Boris Johnson

“Mpango wa kupinga makubaliano ya Brexit wake Johnson utaaminisha waut kupoteza ajira, gharama kubwa madukani na kuhatarisha kuuzwa kwa huduma ya afya ya kitaifa NHS kwa mashirika ya Marekani katika makubaliano na Donald Trump,” Kiongozi huyo wa Leba ameendelea kusema.

“Raia wanastahili kuamua nani awe waziri mkuu katika uchaguzi mkuu,” ameongeza.

Boris Johnson's family - father Stanley, sister Rachel and fellow Tory MP Jo - attended the announcement
Image captionFamilia ya Boris – Babake Stanley na dadake Rachel na mbunge mwenza wa Conservative Jo- wakati wa tangazo la ushindi

Waziri wa kwanza wa Uskotchi Nicola Sturgeon amempongeza Johnson, lakini amesema “ana wasiwasi mkubwa” kuhusu Boris kuwa waziri mkuu.

Changamoto inaanza wakati Johnson apata ushindi

Laura Kuenssberg, Mhariri wa BBC wa kisiasa

Boris Johnson atakuwa waziri mkuu mpya Uingereza.

Kauli ambayo inaweza kufurahisha au kuogopesha. Kauli ambayo anaeleza kwamba miezi 12 iliyopita hata wafuasi wake sugu hawange weza kuliamini hilo.

Lakini sio kauli kavu tu, pengine sio jambo la kawaida kisiasa, ambalo huenda lisikere kwa namna yoyote.

Kwa vyovyote vile unvayomtazama Boris Johnson, yeye ni mwanasiasa ambaye sio rahisi kumpuuza.

Huyu ni mtu ambaye hata utotoni mwake alitaka kuwa ‘mfalme wa dunia’.

Sasa ni mfalme wa chama ha Conservative, na wanaoipigia upatu Brexit, ndio mahakimu.

brexit

Changamoto zilizoko ni za kiwango cha kihistoria.

Boris anaipokea serikali ambayo haina uwingi, ilio na siasa ziliyoachanganyika na sera ambayo katika miaka mitatu ijayo Uingereza na Brussels imeshindwa kuitatua.

Na yeye ni mwanasiasa, ambaye hata washirika wake wanaoshangazwa na kipaji chake wanakiri hung’ang’ana kutoa maamuzi kwa wepesi.

Mojawapo ya wafuasi wake alitamka leo asubuhi pakisubiriwa tangazo la ushindi: “Changamoto inaanza sasa.”

chanzo: bbc

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.