Theresa May ajiuzulu rasmi na kutoa nafasi ya kuthibitishwa Johnson kama Waziri Mkuu

Boris Johnson amewasili katika kasri la Buckingham ambalo ndiyo makao makuu ya Malkia Elizabeth wa Pili ili athibitishwe rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.

Familia ya kifalme imethibitisha kwamba malkia tayari ameshakubali kujiuzulu kwa Theresa May, waziri mkuu aliyekabiliwa na shinikizo la kujiuzulu baada ya kushindwa kulishawishi bunge kuyakubali makubaliano yake ya Uingereza kujiondoa kutoka kwenye Umoja wa Ulaya aliyoafikiana na umoja huo. Johnson anatazamiwa kuzungumza mbele ya makao makuu ya Waziri Mkuu yaliyoko Downing Street baadae leo. Kabla ya kuelekea kukutana na Malkia,

May alimtaka Johnson kutafuta Brexit ambayo inaweza kuleta maelewano ya kisiasa Uingereza. May amesema anajivunia rekodi yake ya kuimarisha uchumi na kufanyia mabadiliko katika huduma za umma.

chanzo: dw swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.