Antoine Griezmann: Kuna uwezekano La Liga kuzuia uhamisho wake kutoka Barcelona kwenda Atletico Madrid

Antoine Griezmann

Usajili wa Antoine Griezmann kwenda Barcelona unaweza kuzuiwa kutokana na mzozo wa malipo.

Uwezekano wa kutokea hatua hiyo umedokezwa na Raisi wa ligi kuu ya Uhispania maarufu La Liga, Javier Tebas.

Klabu aliyotoka Griezmann, Atletico Madrid ilituma malalamiko baada ya Barcelona kutangaza kumsajili Griezmann kwa kukubali kutoa kitita cha euro milioni 120 kama matakwa ya mkataba wa mchezaji huyo ulivyoainisha mnamo Julai 12.

Bei ya mchezaji huyo kimkataba ilishuka kutoka euro milioni 200 mpaka milioni 120 ilipotimu Julai Mosi.

Hata hivyo, Atletico wanaamini kuwa Barca na Griezmann walikubaliana kuhusu usajili mapema mwaka huu na kususbiri ifike Julai Mosi ili bei yake ipungue.

“Inawezeka kuzuia uhamisho wa mchezaji,” Tebas ameuambia mtandao wa Onda Cero.

“La Liga itabidi iamue nini cha kufanyika katika sakata hili.”

Griezmann tayari ameshacheza mchezo mmoja wa kirafiki na klabu yake mpya ya Barcelona, ambapo walifungwa 2-1 na Chelsea nchini Japan.

Tebas amesema: “[Atletico] wamewasilisha malalamiko yao na wameonesha namna gani kuna mashaka ya kuwapatia Barcelona leseni ya Griezmann.

“Tayari kuna mchakato wa kulitatua hili, na wale ambao wanalisimamia itabidi waeleze namna ya utatuzi wake.”

Atletico iliripoti Barcelona kwa chombo kinachosimamia soka duniani Fifa kwa madai ya kumfuata kinyume cha sheria Griezmann mwezi Disemba 2017.

Mchezaji huyo alikataa kujiunga na Barcelona mwaka mmoja uliopita.

Atletico hata hivyo wanadai kuwa Barca walimfuata mchezaji huyo mwezi Machi mwaka huu na kufikia makubaliano yam domo. Atletico imewashutumu mabingwa hao wa Uhispania kwa kuwadharau

chanzo: bbc

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.