Korea Kaskazini yarusha makombora mawili

Korea Kusini imesema jirani yake Korea Kaskazini imerusha makombora mawili yaliyoanguka katika Bahari ya Mashariki ambayo pia inajulikana kama Bahari ya Japan.

Korea Kaskazini imechukua hatua hiyo baada ya kuionya Korea Kusini, dhidi ya mazoezi ya kijeshi inayotarajia kufanya pamoja na Marekani mwezi ujao. Korea Kaskazini pia imeonya kwamba mazoezi hayo ya kijeshi yanaweza kuathiri mipango ya kuanzisha tena mazungumzo na Marekani, kuhusu nchi hiyo kusimamisha shughuli zake za kinyuklia. Korea Kusini imesema bado haijulikani kama Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alisimamia kurushwa kwa makombora hayo. Afisa mmoja ameliambia shirika la habari la AFP, kwamba uchunguzi wa pamoja na Marekani umeshaanza kufanyika. Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema hatua ya Korea Kaskazini kufyatua makombora hayo mawili ni ya kusikitisha.

chanzo: abc nws

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.