Je Trump na Boris wana mtindo sawa uongozini?

Uhusiano kati ya Uingereza na Marekani utakuwa ni wa “kusisimua” kwani sasa Boris Johnson ndiye anayekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza katika Ofisi za Downing Street, amesema Balozi wa Marekani nchini Uingereza.

Balozi Woody Johnson ameiambia BBC kuwa Trump na Boris wanafanana kwa mambo mengi katika mtindo wao wa uongozi na shauku ya kutaka “mambo yafanyike”.

Alikwepa kujibu kuhusu ukosoaji wa Waziri Mkuu dhidi ya Bwana Trump alipokuwa Meya wa London ambapo alimuita Trump “mjinga aliye na upumbavu”.

Na amesema kuwa uwezo wa Uingereza wa kupata mkataba wa biashara na Marekani hauwezi kuathirika iwapo itashindwa kufikia mkataba wa kujitenga na Muungano wa Ulaya-Brexit.

Rais wa Marekani ameelezea kuafiki kupanda mamlakani kwa Boris Johnson , akisema kuwa atafanya “kazi nzuri” na hata akasema Boris ni ” Trump wa Uingereza”.

Trump ambaye anaunga mkono Brexit, alikuwa mkosoaji wa mazungumzo ya waziri mkuu wa Uingereza aliyeondoka madarakani Theresa May na Muungano wa Ulaya(EU).

Balozi wa Marekani nchini Uingereza ,Woody Johnson amesema ''Ninadhani kile ambacho Trump anataka ndio kile ambacho waziri mkuu Boris anataka''
Image captionBalozi wa Marekani nchini Uingereza ,Woody Johnson amesema ”Ninadhani kile ambacho Trump anataka ndio kile ambacho waziri mkuu Boris anataka”

Aidha kumekuwa na hali ya wasi wasi juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na misimamo ya rais wa Marekani kuhusu jamii na wahamiaji , huku mzozo wa hivi karibuni ukiwa ni juu ya kuvuja kwa taarifa za kidiplomasia za Uingereza zilizosababisha kujiuzulu kwa Sir Kim Darroch,balozi wa Uingereza mjini Washington.

Woody Johnson ameiambia BBC leo kuwa kazi yake ni kuzingatia “mambo tuliyokubaliana”.

” Tutakuwa na vikwazo vya barababarani , hilo lazima litakuwepo bila shaka ,lakini nchi zetu mbili ni nzuri ,”amesema.

”Ninadhani kile ambacho Trump anataka ndio kile ambacho waziri mkuu Boris anataka” aliongeza.

Mnamo mwaka 2015, Boris Johnson, akiwa Meya wa mji wa London, alisema kuwa madai ya Bwana kwamba baadhi ya maeneo ya jiji la London “huwezi kuyatembelea” ilionyesha “kiwango kikubwa cha ujinga wa kipumbafu ” na kumfanya kuwa mtu asiyekuwa na uwezo wa kuwa rais.

Alipokuwa Meya wa London Boris Jonson aliwahi kumuita alimuita Trump "mjinga aliye na upumbafu".
Image captionAlipokuwa Meya wa London Boris Jonson aliwahi kumuita alimuita Trump “mjinga aliye na upumbafu”.

Lakini balozi wake mjini London Woody Johnson amesema kuwa Trump hajali kauli zake.

” Uhusiano mpya kati ya waziri wenu mkuu na rais wetu…utakuwa ni wa kusisimua,” amesema. ” Uongozi wao unafanana sana. Wote wana mtindo wao wa lakini unafanana – maono ya wazi ambayo wanataka kuyakamilisha.”

Amesema kuwa Uingereza itakuwa ”mstari wa mbele” kuwa na mkata wa biashara pale Brexit itakapotokea na “sio muhimu ” kwa uingereza kuondoka katika Muungano wa Ulaya ikiwa na makubaliano ya kuleta mafanikio.

“Rais Trump atajaribu kusongesha mbele mambo – Uingereza ni mshirika wetu mkubwa katika Usalama na mafanikio . Anafahamu hilo .”

chanzo:bbc

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.