Waziri wa utalii akamatwa kwa utakatishaji fedha

Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini Zimbabwe (ZACC), imemkamata Waziri anayeshughulikia masuala ya mazingira na utalii, Prisca Mupfumira akidaiwa kuhusika katika utakatishaji wa fedha.

ZACC hivi karibuni imepewa kibali cha kukamata watuhumiwa nchini humo, ambapo imeanza na Waziri huyo ambaye anadaiwa kuhusika katika utakatishaji wa kiasi cha Dola za Kimarekani millioni 95.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Justice Loice Matanda-Moyo amethibitisha kuwa Waziri huyo amekamatwa jana, Julai 25 na atafikishwa mahakamani leo, Julai 26.

Bado yuko nasi na anatarajiwa kufikishwa kortini kesho (leo). Anakabiliwa na mashtaka ya rushwa yanayojumuisha dola milioni 95. Baadhi ya makosa hayo ni hutokana na ukaguzi wa NSSA, anadaiwa alifanya makosa mengine katika wizara yake ya sasa (Wizara ya Mazingira, Utalii na Ukarimu)“, amesema Justice Matanda Moyo.

Hivi karibuni, Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa aliwachagua wajumbe wapya 12 wakiongozwa na Justice Loice Matanda-Moyo na kuwapa mamlaka ya kukamata washukiwa wa rushwa

chanzo: east tv

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.