Nini kinachofanyika katika taifa lisilo na uwakilishi wa wanawake bungeni?

“Sio jambo la kawaida kuwa na viwango vya juu vya dhulma dhidi ya wanawake. Sio jambo la kawaida kwamba hatuna wanawake katika mchakato wa kubuni sheria”, anasema Yasmin Bjornum, mwanaharakati wa kutetea usawa wa kijinsia nchini Vanuatu.

Bunge katika nchi yake – ambayo imebuniwa kutokana na visiwa 80 ambavyo umbali wake ni kilomita 1,300 kusini mwa bahari ya Pacifiki – ina jumla ya wabunge 52.

Cha kushangaza ni kuwa wabunge wote ni wanaume – hali inayoifanya kuwa moja ya nchi tatu duniani zilizo na wabunge wnaume pekee.

“Masuala yanayotuhusu hayaangaziwi katika asasi zote za juu nchini zinazofanya maamuzi ya nchi,” anasema Bjornum.

Kukabiliana na hali hiyo mwaka 2016 alianzisha ukimbi wa Sista mtandaoni kwa lengo la kuwahamasisha wanawake wenzake juu ya haki zao, akiwa na matumaini baadhi yao wavutiwa na juhudi hizo na kuungana nae.

Kwa nini ni vigumu kubadili msimao wa wanaume

Hilda Lini
Image caption”Wanaume hufanya maamuzi ya kila kitu nchini Vanuatu,” anasema Hilda Lini

Wanawake wa Vanuatu wanaopania kujiunga siasa wanakabiliwa na vizuizi vya kila aina, hasa ikizingatiwa kuwa baraza la kitamaduni lina jukumu kubwa kuamua masuala ya kijamii katika nchi hiyo – hususan katika maeneo ya vijijini ambako watu wengi wanaishi.

Mabaraza hayo yanaongozwa na wanaume wanaofahamika kama machifu, ambao pia wanapendekeza nani ateuliwe kuwania kiti cha ubunge.

“Vyama vyote vya kisiasa nchini [Vanatu] vinaongozwa na wanaume. wanateua wagombea ambao baadae wanachaguliwa bungeni.

Hatua hiyo imechangia wawakilishi wote bungeni kuwa wanaume,”anasema mbunge wa zamani Bi Hilda Lini.

Lini alikuwa mbunge wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa mwaka 1987 – na alihudumu kwa miaka 11 katika mihula mitatu tofaut – pia ni mmoja wa wanawake watano waliowahi kushikilia wadhifa huo nchini.

Anasema ukosefu wa wanawake katika nafasi muhimu ya kufanya uamuzi umefanya nchi hiyo kukosolewa: “Iliwachukua wanaume miaka tisa kubuni sheria ya kulinda familia nchi Vanuatu” – sheria ambayo ni ya kukabiliana na mzozo wa kinyumbani- na ambayo utekelezwaji wake mpaka sasa unakabiliwa na changamoto.

Cha kushangaza ni kuwa mataifa mengine mawili ambayo pia hayana uwakilishi wa wanawake katika mabunge yao pia yanapatikana katika visiwa vya bahari ya Pacifiki.

Mataifa hayo ni Micronesia na Papua New Guinea.

Juhudi za kukabiliana na ukosefu wa usawa

Nchini Vanuatu wanaume huchukua pesa za wanaweke
Image captionNchini Vanuatu wanaume huchukua pesa za wanaweke

Lakini wanawake wa Vanuatu wameanza harakati za kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijamii na kiuchumi kati ya wanaume na wanawake.

“Tunazingatia maadili ya kikristo kikamilifu. Wanaume wanaamini wao ndio viongozi na wanawake ni wasaidizi wao,”anasema Bjornum, “Kuna mjadala mkali kuhusu dhana hiyo dhidi ya wanawake bungeni.”

Mwandishi wa BBC aliyezuru eneo hilo anasema ni jambo la kawaidi kwa wanaume kuchukua pesa za wanawake.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka (2017), ni 60% ya watu walio na uwezo wa kupata nguvu za umeme majumbani mwao, huku thuluthi tatu ya watoto wakiwa wamedumaa kutokana na ukosefu wa lishe bora.

Benki ya Dunia inasema ipo haja ya kuangazia upya suala la usawa wakijinsia ikiwa taifa hilo lina mpango wa kujiendeleza sasa na siku za usoni.

Dhulma dhidi ya wanawake

Yasmin Bjornum
Image captionYasmin Bjornum anasema kuna uhusiano kati ya ukosefu wa uwakilishi wa wanawake bungeni na dhulma dhidi ya wanawake

Vanuatu ina watu karibu 275,000, na viwango vya unyanyasaji dhidi ya wanawake vinaripotiwa kuwa juu sana.

“Mmoja kati ya wasichana watatu wamewahi kudhulumiwa kingono kabla ya kutimiza miaka 15,” anasema Bjornum, “60% ya watu wanahudumu kifungo jela wapatikana na kosa la uhalifu wa kingono.”

Kulingana na Bjornum, 98% ya visa vya uhalifu wa kingono havifikishwi mahakamani – na vile vinavyoripotiwa mara nyingu husuluhishwa kupitia ”upatanishi wa kitamaduni”: Mkoseaji akitoa zawadi kama (nguruwe), adhabu dhidi yake inapunguzwa.

“Ikiwa hamtaunga mkono usawa wa kijinsia, taifa halitawahi kubadilika. Lakini pia mila na utamaduni umekita mizizi nchini Vanuatu,” anasema Bjornum.

Siasa za siku zijazo

Wasichana hawa watakapokua wakubwa na kupata nafasi ya kupiga kura huenda wakafanya mamuzi yatakayobadili hatma ya baadae ya Vanuatu
Image captionWasichana hawa watakapokua wakubwa na kupata nafasi ya kupiga kura huenda wakafanya mamuzi yatakayobadili hatma ya baadae ya Vanuatu

Lakini huenda mabadiliko yakafikiwa siku zijazo.

Kuna kundi la wanawake ambalo linataka kubadilisha hali ilivyo kwa sasa kwa kubuni chama cha kwanza cha kisiasa cha wanawake nchini Vanuatu.

Chama hicho kinafahamika kama The Leleon Vanua Democratic Party kinacho ongozwa na Bi. Hilda Lini.

Lini anajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu mwaka 2020 na anashinikiza 50% ya viti bungeni vipewe wanawake.

“Tunapigania utekelezaji wa haki ya kikatiba itakayo wawezesha wanaume, wanawake na watu walio na ulemavu kushirikishwa kikamilifu,” anasema.

Chama hicho kunajitahidi kuwashawishi wanawake kugombea viti kadhaa vya ubunge.

Uhuru wa kupiga kura

Wanaume huwaelekeza wanawake katika familia zao wampigie nani kura
Image captionWanaume huwaelekeza wanawake katika familia zao wampigie nani kura

Zamani wanawake walikua wakipiga kura kulingana na maelekezo ya wanaume katika familia zao.

“Tunamwambia mwanamke kura yake ni siri yake. Ni uamuzi wako. Hauhitaji kumwambia mume wako au mtu mwingine yeyote,” anasema Lini.

Clare Beckton, ambaye ni mmoja wa washirikishi wa kuimarisha utawala wa wanawake katika Chuo Kikuu cha Carleton mjini Ottawa, Canada, anasema “Ukitenga 50% ya watu katikaserikali , inamaanisha hautakuwa na ufahamu wa kutosha wa masuala yanayowakabili.”

Ni mataifa matatu pekee duniani yalio na zaidi ya 50% ya wanawake bungeni, kwa mujibu wa data ya muungano wa mabunge: Rwanda (61%), Cuba (53.2%) na Bolivia (53.1%).

Changamoto kubwa kwa Vanuatu ni kukabiliana na maadili ya kitamaduni – ambayo hayatilii maanani mchango wa wanawake katika uongozi.

Matumaini ya siku zijazo

Hilda Lini akiwa na wanachama wengine wa chama chake
Image captionWanasiasa wanawake nchini Vanuatu wanataka wachaguliwe, kwa hiyo wamebuni chama chao kinacho ongozwa na Hilda Lini (kushoto) kama mgombea mkuu

Kulingana na waangalizi nchini, wanawake wa kila umri wameonesha ari ya kuleta mabadiliko ya kisiasa na kijamii, lakini ni wazee wanao ongoza vikao hivyo vya kujadili masuala hayo.”Ni wao walio katika nafasi ya kufanya hivyo. Wanashirikiana na wanawake wa umri wa makamo,” anasena Yasmin Bjornum,”Wanawake wazee wakiongoza vugu vugu la wanawake watawashawishi wanaume kusikiliza ajenda yao.”Lini anamini “muda wa mabadiliko umewadia”, na mtazamo wake uko wazi: “50% ya bunge iwe wanawake. Wanawake wawe na usemi katika chakatio wa kubuni sheria ya nchi.”

chanzo: bbc swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.