Marekani yatoa kibali cha kukamatwa meli ya Iran

Wizara ya sheria ya Marekani imetoa kibali cha serikali jana kuikamata meli ya mafuta grace 1 , ambayo ni meli ya mafuta ya Iran.

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya jaji katika mahakama ya Gibraltar kuruhusu kuachiwa kwa meli hiyo iliyokamatwa licha ya juhudi za kisheria za marekani kuizuwia. Meli hiyo ilikamatwa Gibraltar na jeshi la majini la uingereza Julai 4 kwa tuhuma za kukiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa kupeleka mafuta nchini Syria. Marekani inadai kwamba meli hiyo , ikiwa ni pamoja na mafuta yake yote iliyobeba na kiasi ya cha dola 995,000 ni lazima kuzuiwa. Meli hiyo ya Iran imebadilisha mwelekeo jana, lakini nanga yake bado iko chini nje kidogo ya Gibraltar na haifahamiki iwapo iko tayari kuondoka

chanzo: DW swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.