Mlipuko mwingine wa lori la mafuta waua 18

Siku chache baada ya ajali kubwa ya mlipuko wa moto wa gari la mafuta kutokea mkoani Morogoro nchini Tanzania na kuua watu zaidi ya 80, tukio linalofanana na hilohilo limetokea nchini Uganda na kuua watu 18.

Msemaji wa jeshi la Polisi nchini Uganda, Fred Enanga amesema kuwa jana jumapili majira ya saa kumi jioni tenki la mafuta lilipuka katika soko la Rubirizi ,Kyambura magharibi mwa Uganda, ambapo dereva wa lori la mafuta lililokuwa linatokea maeneo ya Mbarara kwenda Kasese karibu na mpaka DRC, kuacha njia na kugonga daladala ndogo za abiria mbili na gari ndogo moja na zote kushika moto na kulipuka gari hilo la mafuta kulipuka hapohapo.

Mpaka sasa watu 10 ndio wameweza kutambuliwa huku miili mingine 8 inasubiri majibu ya vipimo vya vina saba kutoka kwa jamaa zao ili waweze kutambulika.

Athari nyingine zilizopatikana katika ajali hiyo ni maduka yapatayo 25 yameateketea pamoja na vitu vyake vyote ndani.

chanzo:bbc swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.