Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte kujiuzulu leo

Waziri mkuu wa Italia Giuseppe Conte amesema atajiuzulu baadaye leo kufuatia uamuzi wa chama tawala cha Ligi kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani katika muungano huo unaounda serikali.

Akilihutubia bunge kuhusiana na mzozo huo wa kisiasa uliozushwa na chama cha Ligi, Conte amesema atakabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa rais Sergio Mattarella, ambae ataamua iwapo anataka kuitisha uchaguzi wa mapema ama kujaribu kuunda muungano mpya wa serikali. Akiwa mkuu wa nchi Matarrella anaweza kumuomba Conte kuendelea na wadhifa huo na kujaribu kutafuta mbadala wa wingi katika bunge, ama kukubali kujiuzulu kwake na kuangalia iwapo baadhi ya viongozi wengine wanaweza kuunda muungano mbadala wa uongozi. Ikishindikana, Mattarella anaweza kulivunja bunge , na kuiweka nchi hiyo katika uchaguzi wa mapema mwezi Oktoba

chanzo:DW swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.