Mamia ya waandamanaji kushindikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania

Zaidi ya watu 100 jijini Dar es Salaam wameandamana mpaka ubalozi wa Afrika Kusini wakishinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania inayozuiliwa jijini Johannesburg.

Waandamanaji hao waliokuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kwa lugha za kingereza na kiswahili wamefika katika ubalozi huo uliopo kati kati ya jiji asubuhi ya leo.

Ndege hiyo iliyokuwa inatoka Johannesburg, Afrika Kusini kwenda jijini Dar es Salaam, Tanzania Agosti 23, 2019 ilizuiwa kuruka kwa amri ya Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng.

mAANDAMANO

Haijulikani watu hao walitumia njia gani kujikusanya ama wanafungamana na kundi gani la kisiasa ama kiharakati.

Ndege hiyo aina ya Airbus A220-300 imeshikiliwa katika uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg kwa amri ya mahakama.

Air Tanzania

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania Dk Hassan Abbas hivi karibuni amefafanua kuwa ndege hiyo imeshikiliwa kutokana na kesi ya fidia inayomhusu raia wa Afrika Kusini Bwana Hermanus Steyn na Serikali ya Tanzania.

Mtu huyo ambaye alikuwa anamiliki ardhi, mifugo na mali nyingi, zilitaifishwa na serikali ya Tanzania miaka ya 1980 na walifikia makubaliana na serikali ya Tanzania.

Amesema ilipofika miaka ya 1990 walikubaliana fidia atakayolipwa, miaka ya 2000 akalipwa na kuna kiasi kilichobaki ambacho mhusika amefungua kesi akitaka amaliziwe kulipwa.

Aidha Dk Abbas amesema mdai huyo amekwenda Afrika Kusini kwa taratibu za mahakama, akibainisha kuwa zipo nchi ambazo mtu anaruhusiwa kuiomba hukumu ya nchi nyingine itekelezwe kwenye nchi aliyopo, akisisitiza kuwa ni taratibu za kawaida kwenye sheria.

Tayari timu ya wanasheria wakiongozwa na wanasheria Mkuu wa Tanzania Profesa Adelardus Kilangi wapo nchini Afrika Kusini kushughulikia kesi hiyo ili ndege irejee angani.

Hii ni ndege ya pili ya Tanzania iliyonunuliwa na serikali ya raisi John Magufuli kushikiliwa kutokana na madeni ya nyuma. Ndege ya kwanza kushikiliwa ilikuwa Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017.

chanzo: BBC swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.