Urusi na Uturuki kuchukua hatua za pamoja Idlib

Uturuki na Urusi zimekubaliana kushirikiana kupunguza mashambulizi ya serikali ya Syria katika mkoa unaodhibitiwa na waasi wa Idlib.

Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan amekosoa mashambulizi yanayofanywa na vikosi vya serikali ya Syria kwa msaada wa Urusi katika mkoa huo, akisema yanavuruga utulivu ulioweza kupatikana katika eneo hilo. Mnamo mwezi Septemba Uturuki na Urusi zilikubaliana kusitisha mapigano katika eneo hilo. Akiwa pembezoni mwa Erdogan mjini Moscow hapo jana,katika mkutano wa pamoja na waandishi habari.

Vilevile Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema mashambulizi hayo yana lengo la kupambana na makundi ya kigaidi katika mkoa huo. Putin amewaambia waandishi habari kwamba amekubaliana na Erdogan kufanya kazi pamoja kutuliza hali inayoendelea huko Idlib lakini bila ya kutoa maelezo zaidi.

chanzo: DW swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.