Hasira kali baada ya Bunge kusitishwa Uengereza

Wabunge na wapinzani nchini Uengereza wanaopinga kuidhinishwa Brexit bila mpangilio wameghadhabiswa vikali na uamuzi wa Waziri Mkuu kusitisha bunge.

Wafuasi hao wameaandamana kote nchini, kesi iliowasilishwa dhidi ya hatua hiyo na waraka uliosainiwa na zaidi ya watu milioni moja kupinga hatua hiyo.

Aidha Serikali imesema kuistishwa kwa wiki tano kwa vikao vya bunge mwezi Septemba na Oktoba kutaruhusu muda wa kutosha kujadili Brexit.

Hatahivyo wakosoaji wanasema ni hatua “isio ya kidemokrasi ” kuwazuia wabunge kupinga brexit bila ya mpangilio.

Vilevile Waziri Michael Gove ameiambia BBC kwamba kusitishwa huko kwa bunge kulikoidhinishwa na Malkia siku ya Jumatano ‘bila shaka sio’ hatua ya kisiasa kuzuia upinzani kwa hatua ya Uingereza kujitoa katika Muungano wa Ulaya pasi kuwepo mpangilio.

Anti-Brexit demonstrators in Whitehall
Image captionWaandamanaji wanaopinga Brexit – Uingereza kujitoa katika Muungano wa Ulaya walikusanyika huko Whitehall, karibu na Downing Street

Nae kiongozi wa bunge Michael Gove aliyekuwa katika mkutano na Malkia amesema vikao hivi vya bunge vilikuwa virefu kuwahi kushuhudia katika takriban miaka 400, kwahivyo ni sawa kusitishwa na kuanza kikao kipya.

Kiongozi wa chama cha Leba Jeremy Corbyn ameitaja hatua hiyo kama “pigo na unyakuzi kwa demokrasia yetu” ili kulazimisha Brexit bila ya mpangilieo kwa kuwaacha wabunge pasi kuwana muda wa kutosha kupasisha sheria bungeni. Aliahidi kujaribu kuisitisha hatua hiyo ya kusitishwa kwa bunge.

Na mwanaharakati anayepinga Brexit Gina Miller – aliyewahi kushinda kesi dhidi ya mawaziri kuhusu kipengee cha ‘Article 50’ – amewasilisha ombi la kuikagua sheria dhidi ya uamuzi huo wa Johnson.

A protestor opposing the suspension of Parliament
Image captionOthers gathered outside Parliament late into the evening

Baadhi ya waandamanji waliozungumza na BBC waliashiria kwamba huu ni mwanzo tu wa ukosefu wa utulivu, kukiwa kumepangwa maandamano zaidi mwishoni mwa juma.

chanzo : BBC swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.