Nani atanyakua taji la mchezaji bora Ulaya?

Uefa leo Alhamisi inatarajiwa kumtangaza mchezaji bora wa mwaka wa soka Barani Ulaya .

Waliojumuishwa katika orodha ya kushindania tuzo hiyo ni beki ya Liverpool Virgil van Dijk anawania taji hilo dhidi ya Cristiano Ronaldo wa Juventus na Lionel Messi Barcelona.

Kama Luka Modric alivyofanikiwa kuwaoondoa Ronaldo na Messi katika udhibiti wa tuzo hiyo mwak jana- nae Van Dijk ana matumaini ya kuwapiku nyota hao wa soka kwa kuishindi Liverpool taji hilo mashuhuri.

Linapokuja suala la kuorodhesha wachezaji bora wa kuwania mataji – iwe ni Barani Ulaya au Duniani- Messi na Ronaldo wamejumuishwa katika orodha hizo kwa zaidi ya mwongo mmoja.

Tangu Tuzo ya Uefa ya mchezaji bora wa kiume ilipozinduliwa mwaka 2011, Ronaldo ameshinda mara tatu (2014, 2016, 2017), huku Messi akishinda Tuzo hiyo mara mbili (2011 na 2015).

Wawili hao wanamenyana tena baada ya misimu ya kusisimua ya. Ronaldo aliisaidia Juventus kushinda ligi ya Italia maarufu Serie A nae Messi akaongoza Barcelona kushida ligi ya La Liga .

Virgil Van Dijk

Van Dijk amekuwa baraka kwa Liverpool tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Southamptonna ammekuwa kiungo muhimu kuisaidia kushinda Champions League msimu uliopita na pia kuisaidia kuwania taji ya Ligi ya Premia dhidi ya Manchester Cityhadi mwisho.

Beki huyo hajawahi kushinda tuzo kwa hivyo hatua ya nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi kuwania tuzo dhidi ya Messi na Ronaldo tayari ni mafanikio makubwa.

Katika mashindano yote ameonesha kwa zaidi ya 70% umuhimu wake kama beki.

chanzo: BBC swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.