Virgil van Dijk ajinyakulia taji la mchezaji bora Ulaya

Hatimae Virgil van Dijk awabwaga Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Enzi za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi za kutawala tuzo za mpira zinaendelea kusukumwa ukingoni.

Usiku huu beki huyo wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk amewaangusha Van Dijk amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa bara Ulaya kwa mwaka 2018/19 Van Dijk baada ya kuingoza safu ya ulinzi ya Liverpool kuchukua Champions League msimu uliopita.

Kama Luka Modric alivyofanikiwa kuwaoondoa Ronaldo na Messi katika udhibiti wa tuzo hiyo mwaka jana – Van Dijk amekuwa mtu wa pili kuwapiku nyota hao ambao wametamba kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita.

Virgil Van Dijk

Ni wazi kuwa Van Dijk amekuwa baraka kwa Liverpool tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Southampton na amekuwa kiungo muhimu kuisaidia kushinda Champions League msimu uliopita na pia kuisaidia kuwania taji la Ligi ya Premia dhidi ya Manchester City hadi mwisho.

Kabla ya leo alikuwa hajawahi kutwaa tuzo kubwa yeyote. Lakini usiku huu analala na tuzo mbili; mchezaji bora wa Ulaya na beki bora wa Ulaya.

Cristiano Ronaldo, Lionell Messi, Virgil van Dijk
Image captionEnzi za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi za kutawala tuzo za mpira zinaendelea kusukumwa ukingoni

Takwimu za michezo ya mwaka 2018-19 zinaonesha kuwa Van Dijk aliiwakilisha klabu na taifa lake katika mechi 59.

Alifunga mabao tisa na kusaidia ufungaji wa mabao manne. Pia alichezea Liverpool kwa dakika nyingi zaidi ya mchezaji mwingine yeyote (4,465) .

chanzo: BBC swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.