Trump atengenezwa sanamu

Sanamu ya mbao ya rais wa Marekani imejengwa katika nchi alikozaliwa mkewe ya Slovenia, iliibua maoni tofauti.

Ikiwa na urefu wa karibu futi 26, sanamu hiyo ilijengwa katika ardhi ya kibinafsi na inamuonyesha Donald Trump akiwa na kichwa cha muundo wa mraba na kidevu huku akiwa anyenyenyua kichwa juu.

Msanii aliyeitengeneza ameliambia shirika la habari la AFP kuwa alitaka iwe kama kielelezo cha maoni ya kisasa ya wanaohisi kuwa watawala wa kisiasa hawawajali.

Sanamu hii imewekwa baada ya ile ya mke wa trump, Melania inayomuonyesha akiwa na ulimi uliojaa ndani ya mashavu.

Sanamu ya Melania, iliyochongwa ndani ya mti viungani mwa mji alikozaliwa wa Sevnica, inamuonyesha akiwa amevalia koti la rangi ya blu huku mkono wake ukionyesha angani. baadhi ya wakazi wanaichukulia kama ”aibu”, na wanasema inaonekana zaidi kama katuni kuliko mke wa rais wa Marekani.

Wooden effigy of Donald Trump in Slovene village of Sela pri Kamniku. 29 August 2019

sanamu ya Bwana Trump inamuonyesha akiwa amevalia shati la blu na tai nyekundu, huku akiwa amesimama mithili ya mnara wa uhuru wa New York.

Bwana Schlegl anasema muundo wa ndani ya sanamu ya mbao unairuhusu kubadilika kutoka “sura ya urafiki mnamo siku za kazi za wiki na kuwa na sura ya kutisha sana katika siku za wikendi “, ikiwa ni ishara ya unafiki wa wanasiasa wanaotaka kuonyesha kuwa wanawajali wale wanaohisi kuwa wamesahaulika.

chanzo: BBC swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.